App ya Kitabu cha nyimbo za Tenzi za Rohoni kinakuletea Tenzi ya Kielektronki
App hii inakuwezesha kupata Kitabu cha Tenzi za Rohoni kwa njia ya Kielektroniki na kuweza kukihifadhi kwenye Simu yako.
Ghirex Technology sio mmiliki wa kitabu hiki sisi tunakupa urahisi tu wa kuweza kukipata mtandaoni. Kitabu hiki kina milikiwa na Kanisa la Mennonite Tanzania (KMT) kikiwa na hati miliki inayotambuliwa kisheria chini ya COSOTA.
Hatukusanyi hela yoyote kwenye APP hii.
Kwenye App hii ya Tenzi za Rohoni pia tumekuwekea Imani ya Mitume, Zaburi ya 23, Sala ya Bwana na Neema
============================================================
DIBAJI - (Kama ilivyo kwenye kitabu cha Tenzi za Rohoni)
------------
WACHAPAJI wanaziombea nyimbo hizi kwamba zitakapo imbwa ziwe za kumsifu Mungu wetu anayestahili kusifiwa; tena ziwe nuru ya kuonyesha njia ya Yesu Kristo kwa wote watafutao. Tuimbe sote kwa kuitafakari maana ya maneno, huku tukimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwetu. Kila wimbo una sababu yake na wakati wake wa kufaa kuimbwa. Kwahiyo tuzichague nyimbo za kuimbwa mkutanoni kwa uangalifu na kwa uongozi wa Mungu.
Nyimbo nyingi katika kitabu hiki zimechapwa kutoka kwa Nyimbo (Standard), Kwa kifupi "N.S." nasi twaishukuru "The Society of Promoting Christian Knowledge" na "The Church Missionary Society" kwa ruhusa kuchapa humo nyimbo hizo. Pia twashukuru kupewa ruhusa na "East African Union Mission of Seventh-Day Adventists" kutumia nyimbo chache kutoka kwa Nyimbo za Kristo, kwa kifupi "N.K."